Ni namna ya kupiga muziki/kuimba kwa namba, kuzipa noti namba. Hii ni lugha ya muziki na
ambayo inakuwezesha wewe mpigaji wa kinanda au chombo kingine cha muziki
au mwimbaji kuwasiliana na kuelewana na mwenzako. Mfumo wa nyimbo huwa katika mtiririko
fulani wa namba na hivyo kuleta maana iliyokusudiwa.
Muziki umegawanyika katika namna
mbili; kuna muziki wa kusoma (music by
Sight) na muziki wa kusikia (music
by Ear). Muziki wa kusoma ni ule unaotumia nota/staff notation, lakini muziki wa sikio ni ule ambao unajua/ kupiga
bila kusoma nota ila unafuata taratibu zote kama za Yule anayesoma ila wewe
unatumia sikio lako katika kuukamilisha muziki huo.
Hii ndio aina ya muziki
inayotumika kwa watu wengi zaidi duniani, na inarahisisha kwa maana ule wa
kusoma humuhitaji mtu atumie muda zaidi hata wa kuwa darasani kuliko huu wa
kupiga kwa sikio. Aina zote ni za muhimu sana na ni za heshima na za kukubalika
duniani kote; kumbuka muziki ni lugha hivyo lazima ujue jinsi ya kuwasiliana,
hivyo number system ni mojawapo ya
maneno au misamiati inayokuwezesha kuwasiliana kwa ufasaha katika lugha hii ya
muziki.
Lakini
ili uweze kupiga wimbo wowote/au kuimba ni lazima ujue “number system” kwa sababu ndipo
mahali pekee unapoweza kuunganisha kodi zako na zikaleta maana, na hivyo kupiga
wimbo wako: hivyo chukua muda wa kutosha kujifunza na kuelewa somo hili, kwa
sababu masomo ya mbele yanategemea sana uelewa wako juu ya somo hili la “number
system.”
Fanyia mazoezi kwenye funguo zote
{DO} – {RE} – {MI} – {FA} – {SO} – {LA} –
{TI} – {DO}
{1}
{2} {3} {4}
{5} {6} {7}
{1}
Mwimbaji ni muhimu sana pia kujua number sytem ili ikurahisishie namna ya kupangilia sauti vizuri.
MUONDOKO/ MOVEMENT
Movement/muondoko
ni hatua unazopiga au unazotakiwa kuzizingatia unapohama kutoka noti moja
kwenda nyingine ili uweze kupata namba
system yako kwenye ufunguo wowote ule bila hata ya kufundishwa au kuwa na
mwalimu, hivyo unatakiwa ufuate masharti yafuatayo.
Kwenye
muondoko huwa tuna vitu viwili vya kuvizingatia. FULL TONE/WHOLE TONE (TONI NZIMA), na HALF TONE (NUSU TONI)
FULL STEP/ WHOLE STEP (HATUA NZIMA)- Ni pale
unaporuka noti moja katikati, iwe kwa kupanda au kushuka, (muondoko wa Hatua
nzima). Kwa mfano uko C na ukapanda toni nzima utaenda D. ukiwa hapo hapo C
ukashuka toni nzima utaenda B flat/A sharp. Au uko F#/Gb ukapanda full basi
utaenda G#Ab na ukishuka full toni utaenda E. Ukiwa A ukapanda Full utaenda B,
ukishuka full pia utafikia G. vivyo hivyo na kwa funguo zingine, kumbuka FULL
maana yake UNAACHA NOTI MOJA KATIKATI
HALF STEP (NUSU HATUA)- Ni pale
ambapo hauruki noti yoyote, iwe kwa kupanda au kushuka (muondoko wa Nusu hatua).
Kwa mfano uko C na ukapanda nusu toni utaenda C#/Db. ukiwa hapo hapo C ukashuka
nusu toni utaenda B. Au uko A#/Bb ukapanda Half (nusu toni) basi utaenda B na
ukishuka Half tone utaenda A. Ukiwa E
ukapanda Half (nusu) utaenda F, ukishuka nusu toni utafikia Eb/D#. vivyo hivyo
na kwa funguo zingine, kumbuka HALF maana yake HAUACHI/HAURUKI NOTI YOYOTE
KATIKATI.
HIVYO BASI ukiwa kwenye ufunguo
wako husika na unataka upate hiyo namba system; ni muhimu kuzingatia Formula
hii/ utaratibu huu wa HALF na FULL STEP, hii itakuwezesha kupiga key/ ufunguo
wowote ule hata kama hujawahi kuupiga au kufundishwa. Kumbuka cha kwanza ni
kuchagua ufunguo husika, mfano labda unataka kupiga ufunguo A, au F# hivyo
unaenda kwenye ufunguo husika na unaanza kutafuta number system yake ili uweze
kupiga wimbo wowote ule.
Tufuatane hapa sasa kwa umakini kabla
hujasoma mchoro.
1 kwenda
2= FULL STEP
2 kwenda
3= FULL STEP
3 kwenda
4= HALF STEP
4 kwenda
5= FULL STEP
5 kwenda
6= FULL STEP
6 kwenda
7= FULL STEP
7 kwenda
1= HALF STEP
ZINGATIA; katika muondoko wetu/movement kuna
nusu hatua mbili tu ambazo ni kutoka 3 kwenda 4 na kutoka 7 kwenda 1 basi,
zingine zote zilizobaki na hatua nzima. Formula hii/ utaratibu huu unatumika
kwenye funguo zote/keys zote, Fanyia mazoezi kwenye funguo zote (katika chombo chako unachopiga).
Kama una maswali au mchango wowote waweza changia hapo chini. Endelela kuwa nasi na Mungu akubariki sana.
Sephone Sospeter.
