Muziki ni kitu kipana sana na huweza kufafanuliwa kwa jinsi tofauti tofauti, maana mbalimbali zimeweza kutolewa na wataalam mbalimbali na maana zote hizi zina mlengo mmoja wa kuufafanua muziki.
Kamusi
ya Webster II ya New Riverside University inatafsiri muziki kuwa ni Sanaa ya kupanga sauti katika mtiririko maalum
ili kutengeneza muundo endelevu.
Kamusi
ya Oxford toleo la 7 inafafanua; muziki ni sauti zilizopangiliwa vizuri kiasi
ambacho zinafurahisha kusikiliza. Inaendelea kusema watu wanaweza kuimba muziki
au kuupiga kwa kutumia ala za musiki.
Maana zote
hizo na nyingine nyingi ziko sahihi kabisa. Kwa upande wangu ninaweza kuuelezea
Muziki kuwa ni; sauti za binadamu au za ala za muziki {au zote kwa pamoja}
zisikikazo kwa mpangilio maalum na
kwa madhumuni maalum; mf;
kuburudisha, kuelimisha, kuonya, nk.
Muziki ni
kitu chenye nguvu kubwa sana na hivyo kuwa chanzo cha mambo makubwa tofauti
kutokea; kwa mfano jeshini nyimbo hutumika sana katika kutia moyo wa kupigana
na adui na hatimaye kushinda. Muziki huweza kuleta faraja kwa mtu aliyeumizwa
na vitu mbalibali mfano kazini kwake au katika mahusiano yake na marafiki au
jamii kwa ujumla.
Katika
kitabu chake cha “Jifunze gitaa”, ndugu Lister Nhukuwalla anafafanua zaidi kwa
kusema “Muziki ni kitu ambacho huvuta usikivu wa mwanadamu. Maana upigaji wake
na upangaji wa vyobo humfanya anayevitumia vimfikishe anakotaka au msikilizaji
avutwe na muziki huo.
Katika
kuielezea maana ya muziki hapo juu nimesisitiza maneno manne {sauti za
binadamu, ala za muziki, mpangilio, na madhumuni } kwa sababu ni ya muhimu sana
katika muziki.
Sauti za binadamu; katika muziki sauti za binadamu
huweza kupangwa katika mpangilio maalum na wenye kuvutia kusikiliza. Kuna
mpangilio wa takriban sauti nne; sauti ya kwanza, ya pili, ya tatu, nay a nne.
Sauti hizi zote hupangiliwa kitaalam na hivyo huweza kuleta msikiko mzuri na wa
kupendeza masikioni mwa msikilizaji. Kuna mbinu nyingi na nzuri hutumika katika
kuzipanga sauti hizi na hivyo kuleta radha nzuri masikioni mwa msikilizaji n
ahata mwimbaji mwenyewe. Katika kitabu hiki hatutaangalia kwa undani sana jinsi
ya kuimba kwa hivyo kwa uchache utakuwa umepata nini umuhiu wa sauti za
binadamu katika kuunda muziki.
Mpangilio; dhana hii ya mpangilio ni pan asana
na inahusisha uundaji mzima wa muziki. kwa mfano lazima ujue ni vyombo vya aina
gani utavitumia katika muziki wako au wimbo, ni sauti zipi utaimba, pia lazima
ujue utapigaje vyombo vyako mfano kinanda au gitaa utavipiga kwa wakati gani,
na kwa nidhamu ipi; mfano katika
mpangilio wako labda unaweza kuanza kwa kupiga Kodi kuu {Major chord} na kuishia na kodi ndogo {Minor chord}.
Au pia ni
jinsi gani mtaachiana nafasi ya kupiga kila chombo katika nidgamu inayoeleweka,
kwa mfano wakati waimbaji wanaimba gitaa ya solo inaweza kuwa chini nap engine
vyombo vingine vikawa katika hali ya utulivu mkubwa na baadae waimbaji
wakinyamaza kuupisha vyombo vya muziki hapo gitaa ya solo inaweza ikapanda
kidogo na kusikika likiwaongoza vyombo vingine kama kinanda na besi gitaa. Kwa
hiyo mpangilio ni wa muhimu sana ili kuweza kuleta maana inayoeleweka kwa
sikilizaji na mwanamuziki mwenyewe pia, pia ni lazima upangilie jinsi korasi au
ubeti utakavyoenda katika wimbo na vyombo gani vya muziki utakavyotumia pia.
Madhumuni; dhana hii pia ni ya muhiu sana katika
muziki, kila aina ya muziki auimbao tu inakuwa na maudhui nyuma yake, maudhui
hayo huweza kutofautiana kutoka muziki mmoja na mwingine kutokana na sababu
mbalimbali kama mahitaji ya jamii husika, au kusudi la mwanamuziki wenyewe. Kwa
mfano muziki unaweza kupigwa kwa dhumuni la kuelimisha jamii kwa jambo fulani
mfano; afya, elimu bora, mapenzi, kusifu nchi. Pia muziki unaweza kuwa na
dhuuni la kuchekesha, kumsifu na kumwabudu Mungu, kuonya.
Ala za muziki/vyombo vya muziki; Kuna ala za muziki {vyombo vya
muziki}, za aina mbalimbali, na pia huweza kutofautiana kutoka tamaduni moja na
nyingine pamoja na mazingira ya watu husika. Kwa sababu kitabu hiki kinaangalia
Zaidi chombo kimojawapo cha muziki {kinanda} tutapitia kwa uchache aina
nyingine za vyombo vya muziki kwa sababu vina mahusiano ya karibu sana na
kinanda.
Kuna makundi
manne ya vyombo vya muziki na vimegawanywa kutokana na mlio wa chombo husika
1: Ala za
kupuliza {Aerophones}
Kundi hili
linahusisha vyombo vyote vinavyotoa sauti kwa kutegemea hewa. Mfano wa vyombo
hivyo ni kama tarumbeta, zumari, filimbi, pembe n,k.
2: Ala za
kugonga {Idiophones}
Kundi hili
linahusisha vyombo vyote vinavyotoa mlio kwa kugongwa na kitu kingine kama
chuma, mti n.k. vyombo vinavyoweza kuingia kwenye kundi hili ni kama; Marimba
ya mikono {thumb piano} ambayo hupigwa kwa kutumia vidole gumba. Kifaa kingine
ni marimba ya vibao ambayo hupigwa kutumia vibao.
3: Ala za
kuwambwa {Membranophones}
Vyombo
vinavyohusihwa humu ni vile vinavyotoa sauti yake kutokana na mtetemo wa ngozi.
Ngoma ndicho chombo kinachoingia sana katika kundi hili; zote ngoma za asili na
hata zile za kigeni.
4: Ala za
nyuzi {Chordophones}
Ala
zinazoingia katika kundi hili ni zile zilizotengenezwa kwa nyuzi ambazo ndizo
hutoa mlio. Ala hizo kama; zeze, gitaa, violincello, violin na kinanda cha
piano.
Kama una maswali au mchango wowote waweza changia hapo kwenye kibox chini. Endelela kuwa nasi na Mungu akubariki sana.
Sephone Sospeter.
Mungu akubariki sana. Kwa lugha nyepesi sana napata maana na radha ile ninayoitaka.
ReplyDeleteNime elewa sana Ubarikiwe sana
ReplyDeleteSafi mwalimu
ReplyDeleteImekaa vizuri
ReplyDeleteIko vizuri
ReplyDelete