Wednesday, 14 February 2018

NUMBER SYSTEM (MFUMO WA NAMBA).









Ni namna ya kupiga muziki/kuimba kwa namba, kuzipa noti namba. Hii ni lugha ya muziki na ambayo inakuwezesha wewe mpigaji wa kinanda au chombo kingine cha muziki au mwimbaji kuwasiliana na kuelewana na mwenzako. Mfumo wa nyimbo huwa katika mtiririko fulani wa namba na hivyo kuleta maana iliyokusudiwa.

Muziki umegawanyika katika namna mbili; kuna muziki wa kusoma (music by Sight) na muziki wa kusikia (music by Ear). Muziki wa kusoma ni ule unaotumia nota/staff notation, lakini muziki wa sikio ni ule ambao unajua/ kupiga bila kusoma nota ila unafuata taratibu zote kama za Yule anayesoma ila wewe unatumia sikio lako katika kuukamilisha muziki huo. 

Hii ndio aina ya muziki inayotumika kwa watu wengi zaidi duniani, na inarahisisha kwa maana ule wa kusoma humuhitaji mtu atumie muda zaidi hata wa kuwa darasani kuliko huu wa kupiga kwa sikio. Aina zote ni za muhimu sana na ni za heshima na za kukubalika duniani kote; kumbuka muziki ni lugha hivyo lazima ujue jinsi ya kuwasiliana, hivyo number system ni mojawapo ya maneno au misamiati inayokuwezesha kuwasiliana kwa ufasaha katika lugha hii ya muziki.

Lakini ili uweze kupiga wimbo wowote/au kuimba ni lazima ujue “number system” kwa sababu ndipo mahali pekee unapoweza kuunganisha kodi zako na zikaleta maana, na hivyo kupiga wimbo wako: hivyo chukua muda wa kutosha kujifunza na kuelewa somo hili, kwa sababu masomo ya mbele yanategemea sana uelewa wako juu ya somo hili la “number system.” 

Fanyia mazoezi kwenye funguo zote

{DO} – {RE} – {MI} – {FA} – {SO} – {LA} – {TI} – {DO}
 {1}       {2}       {3}      {4}      {5}        {6}      {7}      {1}    



Mwimbaji ni muhimu sana pia kujua number sytem ili ikurahisishie namna ya kupangilia sauti vizuri.




MUONDOKO/ MOVEMENT

Movement/muondoko ni hatua unazopiga au unazotakiwa kuzizingatia unapohama kutoka noti moja kwenda  nyingine ili uweze kupata namba system yako kwenye ufunguo wowote ule bila hata ya kufundishwa au kuwa na mwalimu, hivyo unatakiwa ufuate masharti yafuatayo.
Kwenye muondoko huwa tuna vitu viwili vya kuvizingatia. FULL TONE/WHOLE TONE (TONI NZIMA), na HALF TONE (NUSU TONI)

FULL STEP/ WHOLE STEP (HATUA NZIMA)- Ni pale unaporuka noti moja katikati, iwe kwa kupanda au kushuka, (muondoko wa Hatua nzima). Kwa mfano uko C na ukapanda toni nzima utaenda D. ukiwa hapo hapo C ukashuka toni nzima utaenda B flat/A sharp. Au uko F#/Gb ukapanda full basi utaenda G#Ab na ukishuka full toni utaenda E. Ukiwa A ukapanda Full utaenda B, ukishuka full pia utafikia G. vivyo hivyo na kwa funguo zingine, kumbuka FULL maana yake UNAACHA NOTI MOJA KATIKATI


HALF STEP (NUSU HATUA)- Ni pale ambapo hauruki noti yoyote, iwe kwa kupanda au kushuka (muondoko wa Nusu hatua). Kwa mfano uko C na ukapanda nusu toni utaenda C#/Db. ukiwa hapo hapo C ukashuka nusu toni utaenda B. Au uko A#/Bb ukapanda Half (nusu toni) basi utaenda B na ukishuka Half tone utaenda A.  Ukiwa E ukapanda Half (nusu) utaenda F, ukishuka nusu toni utafikia Eb/D#. vivyo hivyo na kwa funguo zingine, kumbuka HALF maana yake HAUACHI/HAURUKI NOTI YOYOTE KATIKATI.


HIVYO BASI ukiwa kwenye ufunguo wako husika na unataka upate hiyo namba system; ni muhimu kuzingatia Formula hii/ utaratibu huu wa HALF na FULL STEP, hii itakuwezesha kupiga key/ ufunguo wowote ule hata kama hujawahi kuupiga au kufundishwa. Kumbuka cha kwanza ni kuchagua ufunguo husika, mfano labda unataka kupiga ufunguo A, au F# hivyo unaenda kwenye ufunguo husika na unaanza kutafuta number system yake ili uweze kupiga wimbo wowote ule.

Tufuatane hapa sasa kwa umakini kabla hujasoma mchoro.

1 kwenda 2= FULL STEP
2 kwenda 3= FULL STEP
3 kwenda 4= HALF STEP
4 kwenda 5= FULL STEP
5 kwenda 6= FULL STEP
6 kwenda 7= FULL STEP
7 kwenda 1= HALF STEP

ZINGATIA; katika muondoko wetu/movement kuna nusu hatua mbili tu ambazo ni kutoka 3 kwenda 4 na kutoka 7 kwenda 1 basi, zingine zote zilizobaki na hatua nzima. Formula hii/ utaratibu huu unatumika kwenye funguo zote/keys zote, Fanyia mazoezi kwenye funguo zote (katika chombo chako unachopiga).


Kama una maswali au mchango wowote waweza changia hapo chini. Endelela kuwa nasi na Mungu akubariki sana. 

Sephone Sospeter.




12 comments:

  1. Sephone ubarikiwe. Nasubiria sana uanze kupost videos ambazo zitakuwa na masomo hayo na illustrations tena kwa lugha ya kiswahili. Nafikiri nitapiga hatua zaidi. Ubarikiwe

    ReplyDelete
  2. Baba nabii mkuu...umeinuliwa sana aseee

    ReplyDelete
  3. Sephone be blessed kwa unachokifanya.Mungu akuinue

    ReplyDelete
  4. Sephone be blessed kwa unachokifanya.Mungu akuinue

    ReplyDelete
  5. Somo liko vizuri,Mungu aendelee kukufunulia zaidi.

    ReplyDelete
  6. nashukuru ila kama itawezekana basi weka noti ya ufunguo E

    ReplyDelete
  7. nashukuru ila kama itawezekana basi weka noti ya ufunguo E

    ReplyDelete
  8. Formula ya upigaji wa kila key ni ipi kwa kwa Do. Re, mi, fa, so, la, ti, do

    ReplyDelete
  9. Nisaidie kitabu cha fingering kwenye kinanda

    ReplyDelete
  10. Naomba formula ya kufaham funguo flat zenye alama b

    ReplyDelete